Muungano wa Sayansi #GatesLetter Big Bet Challenge

  • 0.0/5.0

Language: Swahili

Publication Year: 2015

Sisi katika Muungano wa sayansi ni azimio letu
kwamba miaka kumi na tano kutoka sasa bioteknolojia za kilimo zinazokuzwa
na wanasayansi wa sekta ya umma
zitaleta maendeleo katika maisha ya watu duniani.
Miaka kumi na tano kutoka sasa wakulima wote duniani watapanda mimea ambayo
inahitaji dawa chache za wadudu wa mimea na viongezi vya kemikali.
Nao mchele ndizi na mihogo iliyoimarishwa kibiolojia
itaboresha lishe kwa mabilioni ya watu. 
Mbiringanya na kunde zenye BT zitapunguza matumizi ya dawa za wadudu wa mimea 
hivyo basi kunufaisha wakulima, watumizi wa mazao na mazingira.
Mimea nayo itastawi katika hali ya hewa isiyotabirika
kwa hivyo kuhimili joto ukame wadudu na magonjwa 
na pia kuweza kutumia kwa ufanisi zaidi
rasilimali chache kama nitrojeni na maji.
Sisi katika Muungano wa sayansi ni azimio letu
kwamba katika miaka kumi na tano kutoka sasa watu kutoka kila sehemu 
watakuwa wameweza kutumia mbinu bunifu 
ambazo zitaboresha mazingira, usalama wa chakula 
na pia maisha duniani.

Narrated by: Angela Siele

Special thanks: Tom Mbega

Topic

GMO , Bt

Content Pillars

AfS , Food Security

Focus Area

Agricultural Biotechnology , Agriculture , Science Communication

Keywords

Biotechnology, Insects, Pesticides, Food security, Farmers

Published Date

26 Jan 2015

All Metrics

131 Views

0 Downloads

0 Rating by People

Share this page on